Waziri wa Elimu Julius Ogamba amezitaja ripoti potofu zinazoendelea za kwamba serikali imebatilisha hatua ya kusitishwa kwa watu wanaojiunga na chuo kikuu kama taarifa potofu.
Kulingana na waziri huyo amewataka wakenya kupuuzia taarifa hizo huku akisitiza kuwa kiwango cha chini zaidi cha kujiunga kitasalia kuwa C+ na kwamba wanafunzi wote 246, 391 waliopata alama hiyo katika matokeo ya KCSE ya 2024 wanastahili kujiunga na viuo vikuu.
"Serikali haijabadilisha sera ya kizuizi cha uandikishaji katika chuo kikuu. Sehemu hii ya kukatwa bado inasalia kuwa C+ plus na hapo juu, "
Kiwango cha wastani cha C+ kimekuwa kikomo cha kawaida cha kujiunga na vyuo vikuu vya umma kwa miaka sasa.
NA HARRISON KAZUNGU.