UKOSEFU WA 'HUDUMA CENTER' EGU KAUNTI YA KWALE.
Published on 27/02/2025 12:23
News

Wakaazi wa Kijiji cha Egu kata ndogo ya Taru eneo bunge la kinango kaunti ya kwale,wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa ofisi za huduma center zinazotoa stakabadhi muhimu kwa jamii.

Wakizungumza katika mkutano wa usalama eneo hilo,wakaazi hao  wamelalamika kuwa ofisi za kutoa vyeti muhimu kama vile vya kuzaliwa zinapatikana katika ofisi kuu iliyoko kinango.

Aidha wamesema kuwa umbali wa ofisi hizo umechangia watoto wengi kukosa eneo hilo kukosa vyeti vya kuzaliwa na huduma zingine muhimu.

Wakaazi hao sasa wanaishinikiza serikali na taasisi husika kulivalia njuga swala hilo na kujengewa ofisi hizo karibu na makaazi yao.

"Tunazunguka hatujui tutapata wapi mara kwa mara tunapata shida hiyo tunaomba kama itawezekana tuletewe ofisi hapa samburu si mbali ili tuweze kwenda na tupate birth certificate za watoto wetu."

 

By Peter Joseph.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online