VITA VYA DHULUMA ZA KIJINSIA.
News
Published on 21/02/2025

Waziri wa michezo sanaa na utamaduni kaunti ya Kilifi Dr.Ruth Dama Masha amewasihi viongozi kuwa mstari wa mbele katika kupigana vita dhidi ya dhuluma za Kijinsia.

 

Akizungumza mahojiano ya kipekee, Bi:Ruth ametaja kwa muda mrefu familia nyingi zimekuwa zikipitia changamoto kubwa na kukosa kupata haki hasa kina mama.

 

"Ningependa kuwaanbia viongozi wenzangu tuwe mfano wa kuigwa na tushikane mikono tupige vita hivi vya dhuluma ya kijinsia kuna wenye wanaelewa na kuna wale ambao wanapitia dhuluma hizo na hawajui kama wanadhulumika kwa hiyo sisi viongozi tunalojumu."

 

Aidha ameitaka jamii kuripoti dhuluma wanazopitia ili kupata usaidizi kwa wakati huku akisisitiza kuwa ni lazima jamii irudie na kutumia tamaduni zinafaa ili kuishi kwa hali tulivu na usawa katika jamii.

 

"Tunafahamu kuwa kwa sasa mambo mengi yamebadilika lakini isiwe sababu ya sisi kunyanyasana ni lazima tuzitumie vyema zile tamaduni zetu ambazo tunaona zinatufaa kama jamii na pia kama ulibarikiwa na kipato ujaribu kusaidia na kuuinua wengine"

 

NA HARRISON KAZUNGU.

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online