SURA MPYA YA WALEMAVU LAMU.
News
Published on 20/02/2025

Ni tabasamu kwa jamii inayoishi na changamoto za ulemavu kaunti ya lamu baada ya kupokea vifaa vya kutembelea vitakavyowasaidia kujitegemea katika shuhuli zao za Kila siku.

 

Akizungumza katika hafla ya kupokeza vifaa hivyo ,seneta wa lamu Joseph Githuku amewarai wazazi kutowaficha watoto wanaoishi na changamoto za ulemavu na kuhakikisha wanapata elimu kama njia ya kujitegemea katika maisha Yao ya baadae.

 

"Imefika wakati sasa kila mzazi mwenye mtoto mlemavu kumtoa nje ili ajulikane na kupata msaada na utakaomsaidia kila mtoto anahaki kama wengine na haitakuwa vyema tukiwaficha walemavu"

 

Hata hivyo jamii hiyo imeitaka serikali kuwapa kipao mbele katika nafasi za ajira serikalini kwani wamekuwa wakiachwa nyuma kiamendeleo kutokana na changamoto zao zi kimaumbile.

 

"Hata sisi pia tunaiomba serikali iingiliekati wakati wa kutoa nafasi za kazi itukumbuke muda mwingi tumekuwa tukiachwa kwa hali tuliyonayo"

 

Haya yanajiri wakati serikali ya Kenya kwanza inaangazia pakubwa watu wanaoishi na ulemavu na kupewa kipao mbele .

 

NA HARRISON KAZUNGU.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online