TABASAMU KWA WAFANYIKAZI HUMU NCHINI.
News
Published on 15/02/2025

Ni afueni kwa vijana na wafanyikazi humu nchini baada ya wizara ya leba  kuwahakikishia wanalipwa mishahara na marupurupu iliyoidhinishwa na serikali.

 

Akizungumza na wanahabari kikao Cha kamati ya bunge ya kutathimini utendakazi wa wizara hiyo,Katibu mkuu wa wizara ya leba Shedrack Mwadime,ametoa onyo kwa waajiri wanaolipa wafanyikazi malipo duni watachukuliwa hatua za kisheria.

 

"Ni wakati sasa waajiri wote waamke na kuanza kulipa wafanyikazi wao malipo yanayostahili, sisi kama wizira hatutakuba kamwe wafanyikazi wanyanyaswe kwa kulipwa malipo duni na yeyote atakafanya hivyo kwa waajiri wake tutamchukulia hatua za kisheria"

 

Ni kauli iliyoungwa mkono na mwenyekiti wa kamati ya bunge Runyenjes Erick na kutaja kwamba wataweka mikakati dhabiti ya kuhakisha wakenya wanaotafuta kazi nchi za ughaibuni hawanyanyaswi na waajiri wao huku wizara ya leba ikinakali visa hivyo kupungua kwa kiasi kikubwa.

 

"Tunaishukuru sana baada ya kueka ushirikiano wetu na ufanyikazi mwema tunaona sasa vile visa vya wakenya wanaofanya kazi nchi za nje vimepungua na sisi hatutarudi nyuma kamwe katika kuwatetea watu wetu kwa maana tu kwa ajili yao"

 

Haya yanajiri baada ya kugundulika kuwa wananyanyasika kwa kulipwa mishahara duni na wengine kupoteza maisha yao bila sababu za kimsingi.

 

NA HARRISON KAZUNGU.

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online