Kuna haja ya wananchi kuweza kuhamasishwa kuhusiana na swala la utumiaji wa dawa za kulevya.
Kulingana na Katibu wa maswala ya afya Bi Mary Muthoni amesisitiza wakenya wote hukumu Kali itatolewa kwa Watakao husika na ulanguzi huo wa dawa za kulevya.
"Swala la dawa za kulevya limekuwa donda sugu sana hasa Mombasa na Kenya yote kwa ujumla na imefikia wakati sasa tujumuike pamoja ili tupige vita hivi na yeyote atakayepatikana na hatia atachukuliwa hatua za kisheria"
Aidha ametaja kuna mikoa ambayo imeweza kuathiriwa zaidi na janga hili na kutaja serikali itaandaa uhamasisho zaidi kukinga dawa hizi za kulevya humu nchini.
Amezungumza haya mjini Mombasa ambapo wamehusisha baadhi ya washika dau mbalimbali kuhamasishwa kuhusiana na maswala hayo ya dawa za kulevya.
NA HARRISON KAZUNGU