TUMANI KWA WAKULIMA
News
Published on 03/02/2025

Serikali imenunua zaidi ya mafunia milioni tano ya mbolea kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa upanzi wa mvua ndefu inayotarajiwa kunyesha hivi karibuni.

 

Kulingana Katibu Mkuu wa Kilimo Paul Rono amesema wizara yake imenunua magunia milioni 5.9 ya mbolea kusaidia wakulima.

 

Aidha amesema zaidi ya magunia milioni mbili tayari yamesambazwa kwa bohari na vyama vya ushirika zaidi ya 179 vya Bodi ya Nafaka na Mazao.

 

Usambazaji huu unalenga zaidi kaunti ambazo kwa sasa ziko katika awamu ya upanzi, zikiwemo Bomet, Narok, Kisii, Nyamira, Bungoma na sehemu za Kericho na Nakuru.

 

"Tunawahimiza wakulima kuchukua fursa ya mvua ambayo tayari imeanza kupanda," Rono amesema.

 

Hata hivyo amesema wizara inashirikiana na serikali za kaunti kufungua maduka ya ziada ya maili ya mwisho ili kusaidia wakulima zaidi.

 

Mpango huu unalenga kuboresha upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyingine muhimu za kilimo kama vile mbegu.

 

Kwa upande wa Titus Maiyo, msemaji wa Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao, amewataka wakulima wenye ujumbe wa vocha za kielektroniki kuchukua mbolea zao kwenye sehemu iliyo karibu.

 

Amewahakikishia wakulima kuwa mchakato huo utakuwa wa haraka na ufanisi na kuna mbolea ya kutosha kukidhi mahitaji ya wakulima.

 

NA: HARRISON KAZUNGU

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online