IPOA YASEMA HAINA UWEZO WA KUCHUNGUZA VISA VYA UTEKAJI NYARA NCHINI.
News
Published on 29/01/2025

Licha ya wananchi kuamini kuwa maafisa wa polisi ndio wanaoendeleza visa vya utekaji nyara nchini, tume ya kuchunguza utendakazi wa polisi nchini IPOA wamekiri kwamba hawana uwezo wa kuchunguza visa vya utekaji nyara vinavyoshuhudiwa nchini.

Akizungumza mapema Leo mwenyekiti wa tume hiyo Isaack Hassan,amebaini kwamba idara ya polisi imeshindwa kutoa taarifa muhimu itakayowasaidia kufanya uchunguzi kwa kina.

 

Vile vile amesema  kwamba uchunguzi utaendelea licha ya changamoto hizo huku akisema kuwa kwa sasa kesi kadhaa zimewasilishwa  mahakamani kuhakikisha watekaji nyara hao wanachukuliwa hatua ipasavyo.

 

Haya yanajiri huku taifa likiwa linanyooshewa kidole cha lawama na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na  mataifa ya kigeni wakitaka visa hivyo kusitishwa mara moja na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

 

BY PETER JOSEPH

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online