Ni afueni sasa kwa vijana humu nchini baada ya Shirika la westerwelle foundation kwa ushurikiano na ubalozi wa ujerumani wamezindua rasmi ufunguzi wa shirika Hilo tawi la Mombasa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa shirika hilo Joshua Murima amesema lengo na madhumuni la kuja na shirika hilo ni kuhakisha vijana na wafanyibiashara wadogo wanajifunza programu maalumu za kidijitali zitakazo wasaidia kibiashara na kukuza uchumi humu nchini.
"Tutakachofanya na wale wanataka kuanza kuanzisha biashara zao watapata nafasi za kufanyia biashara zao katika afiasi zetu na pia kupata nafasi ya kujiunga wanajasiriamali wengine humu nchini na hata bara zima la Afrika."
Hata hivyo mkurugenzi huyo ametaja mafunzo hayo yatachukua takribani miezi mitano na watakapohitimu watapewa fursa ya kuendelea kufanya kazi zao katika afisi za shirika hilo na hata kupata nafasi ya kujiunga na wajasirimali kutoka pembe zote za nchi na Afrika kwa jumla.
NA HARRISON KAZUNGU.