Shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI nchini lamtaka Waziri wa huduma za umma serikalini justin Muturi na Inspekta Mkuu wa polisi Douglas Kanja kujiuzulu mara moja.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa mkuu wa dharura katika shirika hilo Francis Auma ametaja hatua ya waziri Muturi ya kususia mkutano wa baraza la mawaziri kama ukiukaji mkubwa sheria za nchini.
Auma aidha amesema huenda Muturi amesalia solemba na mwenye Upweke kwenye baraza la mawaziri baada ya kuibua madai ya utekaji nyara kwa mwanawe .
"Mimi naonelea Muturi angejiuzulu tu haiwezekani wewe ulichaguliwa kuwa waziri na kila wakati uwe kinyume na wenzako wakati wakenya wanahitaji huduma za kuwasaidi"
Vile vile ameweza kuwasuta Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja Mkuu wa kitengo cha Ujasusi Noordin Haji na mkuu wa DCI nchini Mohammed Amin na kushinikiza watatu hao wajiuzulu kwa kushindwa kuthibiti visa vya utekaji nyara nchini.
NA HARRISON KAZUNGU.