Mwanaume aua mke wake maeneo ya Huruma
News
Published on 23/01/2025

Maafisa wa upelelezi wa jinai na mauaji kutoka maeneo ya huruma Nairobi, wanachunguza kisa Cha mwanamme mmoja aliyepatikana na vipande vya mwili wa binadamu kwa gunia.

 

Mshukiwa kwa jina John kiama Wambua mwenye umri wa miaka 29, alikiri kwa maafisa wa polisi kwamba alimuua bibi yake Fridah Munani mwenye umri wa miaka 19.

 

Polisi walifanikiwa kufika kwa nyumba ya mshukiwa na kupata vipande zaidi vya mwili na Kisu kilichokuwa  na alama za damu kinachoshukiwa  kama kifaa kilichotumika kutenda unyama huo.

 

Kulingana na taarifa za polisi ni kwamba mshukiwa anazuiliwa katika kituo Cha polisi akisubiri kufikishwa mahakamani huku vipanda vya mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika makafani ya city..

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online