MUTURI ATAFUNGANYA VIRAGO?
News
Published on 22/01/2025

Waziri wa Utumishi wa Umma Justin Muturi alikosekana katika kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri cha Rais William Ruto mwaka huu kilichofanyika Kakamega State Lodge mnamo Jumanne, Januari 21.

 

Kutokuwepo kwake kulifuatia matamshi yake ya hivi majuzi yaliyolenga utawala wa Rais Ruto kuhusu kushindwa kwake kutatua visa vya utekaji nyara nchini.

 

Kwa mujibu wa habari, Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa Serikali inadaiwa hakualikwa kwenye mkutano huo, jambo ambalo lilizua tetesi za uwezekano wa kutokea mzozo kati yake na rais William Ruto.

 

Na Harrison Kazungu

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online