Ni afueni sasa kwa wakenya wanaotafuta huduma katika ofisi za HUDUMA CENTRE kote nchini baada ya katibu mkuu wa utumishi wa umma Amos Gathecha kuahidi kupiga jeki sekta hiyo kwa kima cha shilingi milioni 500
Akizungumza hapa Mombasa Gathecha amesema kwa muda mrefu sekta hiyo haijakuwa na utendakazi wa viwango vinavyostahili jambo ambalo limelemaza shuhuli za wakenya.
"Tumetenga kima cha shilingi milioni 500 katika mgao wa fedha wa mwaka 2025-2026 ili kuimarisha osifi za huduma na kuzifanya ziwe za kisasa na pia kufanya marekebisho mbalimbali ili walenya wanaotafuta huduma katika ofisi hizo waweze kupata kwa wakati na kwa njia inayofaa"
Aidha amewataka wafanyikazi wote katika afisi hizo kuwajibika zaidi ili wakenya wapate huduma kwa wakati.
NA HARRISON KAZUNGU