Changamoto ibuka za mafuriko kwa wakaazi wa ziwa la ng'ombe
Published on 20/01/2025 10:04
News

Wakaazi wa ziwa la ng'ombe walipata fursa ya kuhudhuria tamasha lililoandaliwa na shirika la dream achievers youth organisation DAYO na kupata ufahamu na hamasisho kuhusu athari za mafuriko hususani msimu wa mvua.

 

 Akizungumza na waandishi wa habari,mratibu wa miradi katika shirika Hilo Susan Langisa,ametaja changamoto kadhaa zinazoshudiwa msimu wa mafuriko akitaja kama mimba za kiholela   zinazoletwa na ukosefu wa upangaji uzazi kwa wakati unaofaa,dhulma za kijinsia mwathiriwa kukosa kupata haki , hata maafa kutokana na mikurupuko ya magonjwa ambapo mgonjwa anakosa kupata tiba za dharura.

 

 Vile vile ameangazia shule nyingi huzama au kufurika maji msimu wa mvua na kuchangia pakubwa wanafunzi wengi kuacha shule na kujiunga na magenge hatari ya kihalifu ambayo husababisha utovu wa usalama kwa wakaazi wa ziwa la ng'ombe.

 

Hata hivyo Mratibu huyo ameweza kunyooshea kidole Cha lawama serikali ya kaunti ya Mombasa kuruhusu mijengo inayo jengwa kiholela bila mipangalio kama sababu kuu inayoleta mafuriko ziwa la ng'ombe.

 

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online