Inspekta generali wa polisi bwana Douglas Kanja amefanya mageuzi katika idara ya polisi nchini hususani kwa maafisa wa nyadhfa za ngazi za juu.
Kanja amesema kwamba mageuzi haya ni mpango wa kulainisha sekta ya idara ya polisi na kufanikisha huduma Bora zaidi kwa wa Kenya.
Aliyekuwa Msemaji wa polisi Daktari Resila Onyango amepewa cheo Cha kamanda wa kikosi Cha polisi cha kidiplomasia na kurithiwa na Michael Nyaga aliyekuwa kamanda wa polisi kaunti ya kiambu.
Aliyekuwa Kamanda wa polisi kitengo Cha kumlinda raisi( presidential escort unit) ndiye kamanda mpya wa Nairobi na kumrithi Adamson Bungei.
Hata hivyo Kaunti ya Mombasa haikusazwa ,aliyekuwa kamanda wa polisi kaunti ya kwale Ali Nuno ndiye kamanda mpya wa Mombasa na kumrithi George Seda ambaye ndiye kamanda mpya wa polisi kaunti ya Nairobi.
Ali Nuno anajulikana kwa msimamo wake wa kukabiliana na magenge hatari likiwemo genge la Gaza Nairobi lilokuwa likihangaisha wakaazi wa Nairobi alipokuw OCPD wa kayole.