MWANGA KWA WANABIASHARA WADOGO.
News
Published on 16/01/2025

Ni afueni sasa kwa wafanyabiashara wadogowado hapa Mombasa baada ya shirika la SISTERS FOR JUSTICE kuja na mbinu ya kuwatafutia haki na kutatua mizozo inayowakabili wafanyabiashara hapa Mombasa.

 

Akizungumza katika kongamano lililowaleta pamoja wafanyabiashara mbalimbali hapa Mombasa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Neila Abdalla ametaja kwamba watashirikiana kwa ukaribu na ofisi za kisheria, wanaharakati na wafanyi bishara hapa  Mombasa kuhamashisha umma jinsi ya kutumia koti ya madai madogo madogo na kupata haki zao.

 

Aidha bi Neila ametaja baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitatua mizozo yao ya mikopo kwa njia isiyofaa na kuwaomba kuwshirikiana na Koti ya madai madogomadogo ili kuepuka kuekeana uhasama.

 

"Hali ya uchumi kwa sasa ni ngumu na kuna hawa wafanyabiashara wadogowado ambao wamekuwa wakikopeshena kwa ajili ya kuendeleza biashara zao ama hata kufanyafa shuhuli mbalimbali ila tumeona ikifika wakati wa kulipana baadhi yao hujipaa wanaingia kwenye mizozo mikubwa wengine wanachukua sheria mikononi ndio maana tumekuja hapa leo ili kuwasaidia wafanyabiashara hao"

 

Kulingana naye  zaidi ya kesi elfu 3 zimeweza kuripotiwa kurahisisha   na kutatuliwa kupitia koti ya madai madogo madogo.

 

Neila aidha ameitaka jamii kujiepusha na mizozo na kukoma kuchukua sheria mikononi huku akisisitiza mwana biashara yeyote mwenye deni na mwengine kutumia njia hiyo ili kutatua kesi hiso kwa njia inayofaa huku akitaja kesi hizo huchukua siku 60 pekee mshtakiwa kupata haki yake.

 

NA HARRISON KAZUNGU 

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online