Maafisa wa usalama kutoka kituo Cha polisi cha Shelly beach timbwani kata ndogo ya likoni wamenasa vifaa vya saluni vinayo aminika kuwa vya uwizi.
Kupitia taarifa za ujasusi kutoka kwa umma,maafisa hao walivamia jumba Moja karibu na ofisi za Jara maeneo ya timbwani na Kunasa vifaa kadhaa na bidhaa tofauti vikiwemo,mafuta ,nywele bandia (wigs),kikausha nywele na vinginevyo.
Hata hivyo wakaazi wa maeneo hayo wamelalamika utovu wa usalama kuwa kero na kudai zaidi ya maduka 5 yamevunjwa na kuwaacha wamiliki wa maduka hayo kukadiria hasara.
NA HARRISON KAZUNGU