HEKO MOMBASA.
News
Published on 15/01/2025

Waziri wa elimu kaunti ya Mombasa Dr Mbwarali kame amesifia matokeo ya KCSE ya watahiniwa wa mwaka 2024 katika shule za umma kaunti ya Mombasa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika shule ya upili ya Alidina,Waziri kame ametaja kwamba mpango wa serikali ya kaunti kukumbatia masomo ya ziada imechangia pakubwa shule za umma kaunti ya Mombasa kuandikisha matokeo Bora.

 

Licha ya matokeo ya wanafunzi 840 kutupuliwa mbali nchini,Waziri ametoa kongole kwa ushirikiano Bora kati ya walimu na wazazi akisema hakuna visa vya udanganyifu vimeshuhudiwa  na matokeo kutupuliwa mbali katika kaunti ya mombasa.

 

 

NA HARRISON KAZUNGU.

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online