Waziri wa Utumishi wa Umma Justin Muturi ameishutumu vilali serikali kwa kile anachodai kuzembea na kutaka majadiliano ya wazi kuhusu utekaji nyara unaoendelea humu nchini.
Kulingana na kiongozi huyo serikali haiwezi kuepuka lawama na kusema haina hatia kuhusu suala hilo ambalo amesisitiza kuwa kuna hatari ya kuitumbukiza nchi katika machafuko.
Hata hivyo amesema jinsi utekaji nyara huo unavyotekelezwa mchana kweupe unathibitisha kuwa kuna baadhi ya watu kutoka serikalini wanohusika katika swala hilo.
“Mimi nafahamu kabisa na nina tajiriba ya kutosha ya uwajibikaji katika utendakazi lakini kwa kuwa mimi pia ni mmoja wa waathiriwa wa kutekwa na kutumikia serikali hii sijapata majibu nimechukua hatua hii isiyo ya kawaida ili suala hilo lijadiliwe kwa uwazi na ukweli kama nchi kwa nia ya kutafuta suluhu la kudumu."
NA HARRISON KAZUNGU.