Waziri wa Elimu, Julius Ogamba atatangaza hii leo ametangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kitaifa Kidato cha Nne (KCSE) 2024, leo, Alhamisi, Januari 9, 2025.
Hafla ya kutangazwa kwa matokeo hayo imefanyika katika Makao Makuu ya Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) Jijini Nairobi.
Kulingana na taarifa kutoka kwa Baraza la mtihani la KNEC Jumla ya watahiniwa 965, 512 waliandika mtihani huo mwaka uliopita wa 2024.
Aidha watahiniwa hao ni wanafunzi waliojiunga na shule ya Sekondari 2021 janga la Covid-19 lilipokuwa linatesa taifa na ulimwengu.
Hata hivyo watahiniwa 1,693, wamepata alama ya A, 246, 391 wakipata alama C+, huku watahiniwa 476,889 wakipata alama ya C- na watahiniwa 605,774 alama ya D+ katika mtihani wa K.C.S.E wa mwaka 2024.
Afisa Mkuu Mtendaji KNEC, Bw David Njengere amesema matokeo ya KCSE 2024 yameandikisha historia ya kipekee nchini ikizingatiwa kuwa watahiniwa hao walijiunga na kidato cha kwanza wakati ambapo kalenda ya masomo ilikuwa imesambaratishwa na virusi vya corona.
“Kundi hili, ambalo lilianza safari ya kujiandaa kuandika KCSE Machi 2021, lilionyesha ustahimilivu na uwezo wa kuhimili mabadiliko katika kipindi kigumu kwenye mfumo wetu wa elimu,” Bw Njengere akasema akihutubu katika makao makuu ya KNEC.
Akilinganisha idadi ya watahiniwa walioandika KCSE 2024 na 2023, afisa huyo alisema mwaka uliopita uliandikisha nyongeza ya asilimia 7.19.
“Mara ya mwisho tuliona ongezeko kama hili ilikuwa mwaka wa 2020,” Njengere akasema.
NA HARRISON KAZUNGU