Baraza la Kitaifa la Mitihani humu nchini (KNEC) limetoa matokeo ya Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi ya 2024 (KPSEA).
Kulingana na taarifa kutoka kwa baraza hilo shule zilizowasilisha watahiniwa kwa ajili ya tathmini sasa zinaweza kufikia ripoti mahususi za mwanafunzi kwenye tovuti ya Tathmini-msingi ya Umahiri (CBA), inayopatikana katika cba.knec.ac.ke.
Mwaka huu jumla ya watahiniwa 1,313,913 walifanya mitihani ya KPSEA.
KNEC imezishauri taasisi zote na hata wazazi kuingia katika tovuti hiyo na kupakua ripoti za watahiniwa wao.
NA HARRISON KAZUNGU