Muungano wa chama cha matibabu humu nchini umepeana makataa ya siku 14 kwa serikali kutimiza ahadi walizokubaliana la sivyo waingie katika mgomo kote nchini.
Akizungumza katika kikao na wanahabari rais wa muungano huo Moses Konde Matole ametaja sekta hiyo imezorota kwa kukosa mikakati dhabiti kutoka kwa serikali.
Aidha ameiomba bodi ya bima ya afya ya SHA kuwapa uwezo wa kutoa huduma zao kulingana na vile inayostahili akitaja jambo litawasaidia wakenya kwa kiwango kikubwa zaidi.
NA HARRISON KAZUNGU.