Sekta ya utalii kaunti ya Mombasa imepingwa jeki zaidi baada ya kampuni ya ndege ya TUI kutoka Uholanzi kurudisha tena safari zake katika kaunti hiyo
Hii ni baada ya kampuni hiyo kusitisha safari zake humu nchini baada ya mkurupuko wa janga la Corona.
Akizungumza baada ya kuipokea ndege hiyo katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa,waziri wa utalii kaunti ya Mombasa Mohammed Osman,amesema hatua hiyo itazidi kuiboresha sekta hiyo hasa msimu huu wa likizo ya mwezi Disemba.
"Ndege hii itasaidia tuweze kupata wazungu wengi kutoka Netherlands directly to Mombasa na hawa walikuwa wanasafiri kuelekea Zanzibar ina maana sasa baada ya miaka sita wameregea Mombasa kwa hivyo kuna matokeo mazuri na inaashiria kuwa kaunti ya Mombasa itakuwa makaazi ya hawa wazungu.
"
Wakati uo huo Osman amedokeza kuwa tayari wanashirikiana na wadau wa sekta ya utalii ikiwemo baraza la utalii la Mombasa ili kuhakikisha sekta hiyo inaboreshwa zaidi.
By Susan Umazi