VIONGOZI WA UDA KUTAKA KUMBANDUA GACHAGUA KAMA NAIBU KINA WA UDA.
News
Published on 23/10/2024

Viongozi  wakuu wa chama tawala cha UDA wameanzisha mpango wa kumuondoa naibu rais aliyebanduliwa Rigathi Gachagua kama naibu kinara wa chama hicho.

 

Kulingana na katiba za chama cha UDA naibu rais kisheria huchukua wadhfa wa naibu kinara wa chama.  

Taarifa zinasema kuwa chama hicho pia kina mpango wa kuongeza nafasi za uongozi wake kwa kuunda nafasi mbili za manaibu vinara wa chama bado haijabainika iwapo mpango huo utafanikiwa huku ikiaminika kuwa viongozi wa UDA wanalenga kumbadilisha gachagua kama naibu kinara wa chama ndani ya mda wa wiki mbili zijazo.

 

Haya yanajiri huku ripoti zikisema kwamba wandani wa rais william Ruto wanataka Kithure Kindiki kuwa naibu kinara wa chama hicho under tu harakati za kumbandua uongozini Gachagua zitakapokamilika.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online