kongamano la kutoa hamasa kwa waandishi wa habari kuhusu masuala ya dhulma za kijinsia katika jamii.
News
Published on 12/09/2024

Shirika la kijamii la Dream achievers  youths organization Dayo,limeandaa kongamano la kutoa hamasa kwa waandishi wa habari kuhusu masuala ya dhulma za kijinsia katika jamii.

 

 Aidha kongamano hilo la siku mbili limehusisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari  lengo kuu likiwa ni kuhakikisha maswala ya dhulma za kijinsia yanaangaziwa zaidi hasa mashinani kupitia vyombo vya habari.

 

Kulingana na Enos opiyo  mratibu katika shirika hilo ametoa wito kwa  wanaharakati wa mashirika mbalimbali kuendeleza hamasa kwa jamii huku akiwaomba wanahabari kuchapisha adhabu watakazopata washukiwa wanaoendeleza dhulma za kijinsia.

 

"Teknolojia ikiwa ni njia ambayo dhulma za kijinsia zinaweza kupitishwa ni jambo ambalo linatukia kila kukicha.Tunahimiza wanaharakati kuzidi kuliongelea na kuhamasisha umma kuhusu swale hilo. Wanahabari pia waendelee kuchapisha habari hasa wakiangazia sheria ambazo miongoni mwao ni sexual offences act,marriage act ,proffesion of traffickingact na nyingine zinazolinda haki za umma."

Kwa upande wake Susan Lankisa ambae ni afisa wa WEZESHA  katika shirika hilo amesema kuwa visa vya dhulma za kijinsia mtandaoni vimeongezeka na kuwataka wanahabari kueleza jamii jinsi gani ya kujilinda mitandaoni.

 

"Kuna aina nyingi ya technology facilitated GBV ambayo hufanyika,violation ni nyingi katika jamii hasa kwa wanawake ambao huacha biashara zao mitandaoni wanapopata dhulma.lengo letu ni kuelimisha wanahabari ili waeneze ujumbe huu kwa jamii jinsi ya kujilinda mitandaoni."

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online