Familia ya mwanabiasha Jimi Wanjigi hatimaye imepata afueni baada ya mahakama kuu kuwazuia polisi kuingia katika makazi yake, kuharibu mali yake na kufanya vitendo vyovyote vya kuwashambulia.
Haya yanajiri baada ya familia hiyo wakiongozwa na mkewe Wanjigi Irene Wanjigi kuwasilisha kesi hiyo mahakamani.
Familia hiyo inadai kuwa polisi walichukua vitu vya thamani vya takariban millioni 70 kutoka kwa nyumba yao wakati wa uvamizi uliofanyika Agosti 8 ambapo baadhi ya maafisa wa usalama wanadaiwa kuvunja milango ya nyumba, kuharibu kamera za cctv , miongoni mwa vyombo vingine vya thamani.
Aidha Familia hiyo imeeleza kuwa maafisa wa usalama wamekua wakiwahangaisha kuanzia mwaka wa 2017 hali inayowapelekea kupata msongo wa mawazo.
Kwa sasa wameitaka serikali kuingilia kati iliwaweze kurudishiwa mali zao zinazodaiwa kuchukuliwa na maafisa wa polisi mnamo agost 8 mwaka huu.