Mwanamume kwa jina Dickson Ndiema anayedaiwa kumchoma moto mwana Olimpiki wa Uganda Rebecca Cheptegei na kusababisha kifo chake, amefariki katika hospitali ya Eldoret.
Ndiema alikuwa akipokea matibabu baada ya kuchomeka asilimia 41 anadaiwa kufariki baada ya kushindwa kupumua.
Ikumbukwe kuwa Ndiema anadaiwa kumvamia mkewe kwa kumwagia petroli na baadae kumchoma huko Trans Nzoia.
Mwili wa Cheptegei unatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi nyumbani kwao Kapkoros nchini Uganda.