MSHUKIWA WA MAUAJI YA KWARE ATOROKA
News
Published on 21/08/2024

Mshukiwa wa mauaji ya watu 42 ambao mili yao ilipatikana katika eneo la Kware  anadaiwa kutoroka kutoka kituo cha polisi cha gigiri kaunti ya Nairobi. 

 

Kulingana na maafisa wa polisi mshukiwa huyo Collins Jumaisi  ametoroka na washukiwa wenza 12 raia  wa Eritrea waliokuwa wakizuiliwa kwa makosa ya kuwa humu nchini kinyume cha sheria.

 

Inaarifiwa kuwa afisa mmoja aliyekuwa amewapelekea kiamsha kinywa kwenye seli yao alfajiri ya leo ndiye aliyegundua washukiwa hao wametoroka .

 

Kufikia sasa maafisa watano wamekamatwa  kuhusiana na tukio hilo huku msako mkali  ukianzishwa.

 

By:Susan Umazi

Comments
Comment sent successfully!