Msemaji wa ikulu Isaac mwaura ameonya kuhusu kuendelea kwa maandamano yanayoongozwa na vijana wa Gen Z akieleza kuwa hali hiyo itachangia kuathirika zaidi kwa uchumi nchini .
"Kwa jumla, nchi imepoteza takriban Shilingi bilioni 6 , kulingana na mamlaka ya ushuru ya Kenya, kutokana na maandamano," alisema.
Mwaura sasa amewaomba wazazi kujadiliana na watoto wao na kuwarai kujiepusha na vurugu zinazoathiri biashara na shughuli za uchumi nchini.
Hata hivyo alisema kuwa serikali inajaribu kusikiliza maoni ya wananchi hasa baada ya kuvunja baraza la mawaziri na kutupilia mbali mswada wa fedha wa 2024,kutia sahihi mswada wa IEBC na kupunguza makadirio ya fedha katika ofisi maalum.
By: Susan Umazi