Raila akashifu kuondolewa kwa Ruto madarakani
News
Published on 18/07/2024

 

Kinara wa chama cha Azimio la umoja Raila Odinga, amesema kuwa kumuondoa Rais William Ruto mamlakani kwa sasa huenda isiwe suluhisho bora kwa nchi ya Kenya.

Akizungumza na wanachama wa (ODM), Odinga alisisitiza kuwa kumuondoa Ruto kutoka madarakani kutapelekea Naibu Rais Rigathi Gachagua kuchukua madaraka na kuendeleza sera mbaya.

"Ruto akiondoka, basi nini? Ruto anaweza kuondoka alafu Gachagua anachukua na kuendelea kutekeleza sera mbaya.

Ruto pia anaweza kusema 'Nimechoka, acheni majenerali wachukue madaraka'  halafu nchi inaanza kupitia yale ambayo Misri ilipitia baada ya Tahrir Square.

'Ruto lazima aondoke' haiwezi kuwa suluhu," Odinga alisema.

Aidha, "Ni wakati wa mgogoro kama huu ambapo nchi inahitaji kuzungumza. Hatufanyi hivi kumwokoa Ruto. Tunafanya hivi kuokoa Kenya.

Majenerali hawana vitoa machozi wala mizinga ya maji ila wana risasi."

Msimamo thabiti wa Odinga unaashiria pengo kubwa ndani ya upinzani, hasa ndani ya mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya .

Mivutano ilifikia kilele chake wakati wa mkutano wa hivi majuzi wa Kundi la Bunge la ODM, ambapo kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, ambaye ni mmoja wa viongozi wa Azimio, alitimuliwa ghafla wakati alipokuwa akitoa hotuba  ya kupinga kujiunga na serikali.

Hapo jana hotuba ya Musyoka ilisambaratishwa na vijana wenye vurugu muda mfupi baada ya kuanza kusoma maazimio, huku Odinga tayari akiwa amejiondoa kwa ajili ya majukumu mengine.

 

By: Susan Umazi

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online