MAAFISA 200 ZAIDI KUWASILI HAITI
News
Published on 16/07/2024

Awamu ya pili  ya maafisa wa polisi  wa Kenya takriban 200 wameelekea nchini Haiti baada ya kusafiri  usiku wa Jumatatu ,Julai 15 2024.

Hii ni baada ya ahadi ya Rais William Ruto kuruhusu maafisa wa Kenya kusaidia katika kuregesha nchi hiyo katika hali ya kawaida.

Haya yanajiri baada ya awamu ya kwanza iliyokuwa na maafisa 400 kusafiri Haiti mapema mwezi jana.

Aidha maafisa zaidi wanatarajiwa kuelekea nchini Haiti ili kuendeleza usalama.

By: Susan Umazi

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online