Rais William Ruto ametia saini kuwa Sheria mswada wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC wa mwaka 2024
News
Published on 09/07/2024

Rais William Ruto ametia saini kuwa Sheria mswada wa tume huru ya uchaguzi na  mipaka, IEBC wa mwaka 2024 mapema hii leo.

Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa KICC na kuhudhuriwa na viongozi wa chama cha azimio akiwemo kinara wa chama hicho Raila Odinga na aliyekuwa makamu wa Rais Kalonzo Musyoka pia walikuwepa.

Kwenye taarifa yake rais Ruto alisema ;

"IEBC inabaki kuwa nguzo ya demokrasia yetu inayohusika na kusimamia uchaguzi wa kawaida katika viwango mbalimbali na kuhakikisha mzunguko wetu wa uchaguzi unasimamiwa kwa uwazi na kusimamiwa kwa njia isyoegemea upande wowote kwa ufanisi ,kwa usahihi na kwa uwajibikaji."

Ili kusaidia kurejesha imani ya wananchi katika mfumo wa uchaguzi,Rais alisema kuwa;

"Tumeweza kuleta pamoja vyama vyote vya kisiasa na jamii ya kiraia ili kuhakikisha kuwa tume mpya ya IEBC itakuwa ya haki na yenye  uwazi."

Mswada huo uliopitishwa na bunge unatokana na mapendekezo ya ripoti ya kamati ya kitaifa ya majadiliano (NADCO).

Sheria hiyo mpya itaweka mfumo wa usimamizi wa uchaguzi nchini, ikiwa ni pamoja na kuandaa njia ya uteuzi wa makamishna wapya wa IEBC.

By:Susan Umazi 

 

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online