Hatua ya Rais William Ruto kupunguza matumizi ya fedha kwenye serikali
News
Published on 05/07/2024

Rais William Ruto ametangaza kuvunjilia mbali mashirika 47 ya serikali, kama njia ya kupunguza matumizi ya pesa.

Akizungumza haya Ijumaa mchana kwenye Ikulu ya Nairobi, Ruto amesema wafanyikazi hao wa mashirika yatakayovunjwa watahamishiwa kwingine.

Aidha Ruto ametangaza kupunguza bajeti ya idara zote za serikali, huku afisi yake ikipunguziwa bajeti kwa asilimia 15.

Mbali na Haya Ruto pia ametaka kusimamishwa kazi kwa Makatibu Tawala Wakuu (CAS).

Kupunguza washauri serikalini kwa angalau asilimia 50 mara moja.

Kuondoa Bajeti katika Ofisi za Mke wa Rais, Mke wa Naibu Rais na Mke wa Waziri Mkuu.

Bajeti za siri katika Ofisi ya Urais pia zimeondolewa.

Bajeti ya ukarabati serikalini itapunguzwa kwa asilimia 50.

 Watumishi wa Umma watakaofikisha umri wa miaka 60 watatakiwa kustaafu mara moja na hakuna nyongeza itakayoruhusiwa.

Kusimamisha ununuzi wa magari mapya serikalini kwa mwaka mmoja, isipokuwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

Usafiri wote usio wa lazima wa maafisa wa serikali pia umesitishwa.

 Hakuna afisa wa serikali au mtumishi wa umma atakayeshiriki katika Harambee.

By: Susan Umazi

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online