BUNGE LA SENETI KUPENDEKEZA FIDIA KWA WAATHIRIWA WA MAANDAMANO
News
Published on 03/07/2024

Bunge la seneti limependekeza kuwaachilia watu wote waliokamatwa na polisi kwa madai ya kupinga na kushirika katika maandamano ya kupinga mswaada wa fedha.

Katika kikao cha Bunge hilo kilichofanywa mapema hii leo bunge hilo pia limeitaka serikali kulipia gharama zote za hospitali na mazishi ya waliofariki kutokana na maandamano hayo.

Spika wa bunge hilo Amason Kingi amewaongoza maseneta hao katika kuwakumbuka na kuwaenzi waliofariki wakati wa maandamano .

Aidha Kingi amesisitiza haja ya uongozi wa taifa kuangazia kikamilifu maswala yanayowasilishwa na vijana wanaoandamana nchini kwa takribani majuma matatu sasa.

By: Susan Umazi

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online