JUMANNE YA MAANDAMANO
News
Published on 03/07/2024

Wafanyibiashara na huduma za usafiri zalemaa katika kaunti mbalimbali hapa nchini kutokana na maandamano yanayoendelea kushuhudiwa sehemu mbalimbali nchini.

Mandamano hayo yanayoongozwa na vijana almaarufu Gen Z wakiendelea kupinga uongozi wa Rais William na kumtaka ajiuzulu kwa kile wanachosema kuwa wamechoka kunyanyaswa.

Jijini Nairobi shughuli kadhaa zimetatizika huku maafisa wa polisi wakiendelea kushika doria na kusambaratisha waandamanaji hao.

Hapa Mombasa magari kadhaa yachomwa moto huku maandamano yakiendelea kushuhudiwa eneo hilo.

Ikumbukwe kuwa Rais William Ruto aliweka bayana kuwa yupo tayari kufanya mazungumzo na vijana hao ili kukomesha utovu wa usalama na kurudisha nchi kwenye hali ya kawaida.

BY:SUSAN UMAZI

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online