WAKAAZI WA KAUNTI YA MOMBASA WAHIMIZWA WAJIUNGE NA MFUMO MPYA WA BIMA YA AFYA
Highlights
Published on 01/07/2024

WRITTEN ON FEBRUARY 17, 2024

Mnamo tarehe 13 Mwezi wa pili mwaka wa 2024, kulikuwa na mkutano wa kuhamasisha uma kuhusiana na ajenda mpya wa bima ya Afya wa SHIF ambao umefanyiwa ukarabati kutoka kwa mfumo wa zamani wa NHIF huku baadhi ya waalikwa na wageni wahudhuria mkutano huo uliofanyika katika shule ya Kiufundi ya Kisauni.

Wawa

Wakazi wakihamasishwa

Kwa mujibu wa wizara ya Afya wadadisi wasema ya kwamba madhumuni yao kubadili na kubuni bima ingine ya Afya nikwamba, bima ya NHIF imekuwa ikilipia kitanda cha mgonjwa hospitalini pekee yake na ilhali mgonjwa inafaa ajukumike ili aweze kununua madawa, huku nako wafungwa gerezani wakiwa wagonjwa hawangeweza kutibiwa na bima hiyo ya NHIF. Aidha pendekezo hili la bima mpya limeboreshwa kiasi ya kwamba ikiwa mfungwa akona bima hii mpya ya SHIF atatibiwa hadi arudi hali ya usawa wa afya, vile vile ni kwamba mgonjwa akiwa sawa bima hii mpya itagharamia matibabu yote ya mgonjwa huyo hadi arudishe afya yake na pengine itahitajika afanyiwe upasuaji huduma hiyo itagharamia matibabu hayo na malazi pia.

a

Wahusika wakuu wakiwa wizara ya Afya iliyotoka makao makuu Jijini Nairobi na kuja Mashinani na kujumlisha uma kuhusiana na uboraji wa bima ya Afya na baadhi ya vipengee kuongezwa kwenye mkataba huo wa bima ya SHIF. Huku wakaazi wakihamasishwa na kuhimizwa wajisajili upya kwa kuwa zile fedha walizo wekeza kwa bima ya NHIF hazijapotea bali ziko zitafanywa kutumwa kwa akaunti mpya ya bima ya afya ya SHIF yenye utakayo jisajili na majina zako.

 

Mipango ya kubuni tume mpya ya bima ya Afya unaendelea na utakuwa wazi kwa uma na wanatarajiwa Tarehe 1 mwezi wa Tatu mfumo huo uwe umeng’oa nanga hadi siku 90 zijazo na Wakenya wataenda katika vituo vya NHIF na kujisajili hadi tarehe 1 mwezi wa saba mwakWakaazi wa Kaunti ya Mombasa wahimizwa wajiunge na mfumo mpyaa huu.

 

IMEANDIKWA NA ELIJAH MUTHINI

Comments

Chat Online