RAIS RUTO AKATAA KUTIA SAINI MSWADA WA PESA
News
Published on 26/06/2024

Rais William Ruto amekataa kutia saini kuwa Sheria  Mswada wa Fedha wa mwaka 2024/25 mchana wa leo.

 

Taarifa kutoka  Ikulu inasema kuwa Muswada huo utarejeshwa Bungeni kabla ya mapumziko leo.

 

Bunge linaweza kurekebisha Mswada huo kwa kuzingatia kutoridhishwa na rais au kuupitisha mara ya pili bila kuufanyia marekebisho.

 

Rais  Ruto ataonyesha maeneo muhimu ambayo yanahitaji kubadilishwa kwenye mswaada huo.

 

Aidha iwapo wabunge watarekebisha mswada huo ili kuafiki kutoridhishwa kwa Rais kikamilifu, spika wa Bunge la taifa atauwasilisha tena kwa rais ili kupatakibali.

 

 Written by: Susan Umazi

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online