Polisi wa Kenya waelekea Haiti
News
Published on 25/06/2024

Awamu ya kwanza ya maafisa wa polisi  wa Kenya takriban 400 wameelekea nchini Haiti baada ya kusafiri  usiku wa Jumatatu ,Juni 24 2024.

Maafisa hao walikusanyika katika chuo cha mafunzo cha polisi cha Embakasi kabla ya kuondoko uwanja wa Jomo Kenyatta saa 7 usiku kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya (KQ).

Wanatarajiwa kuwasili Port-au-Prince hii leo kabla ya kuanza rasmi misheni yao. Katibu wa baraza la mawaziri wa mambo ya ndani Kindiki Kithure, katibu mkuu Raymond Omollo, Inspekta Jenerali Japhet Koome mkurugenzi mkuu mtendaji wa KQ Allan Kilavuka miongoni mwa maafisa wengine wakuu wa polisi walikuwepo kuwaaga maafisa hao.

Hapo awali Rais William Ruto aliahidi kuwa vikosi vyote vya polisi vitaongezwa mishahara pamoja na marupurupu mengine kuanzia mwezi Julai.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online