WANAFUNZI KUANZA LIKIZO FUPI HII LEO
News
Published on 24/06/2024

Wizara ya elimu imetoa ruhusa kwa shule za bweni kuwaruhusu wanafunzi kuanza mapumziko ya likizo fupi hii Leo.

 

 

Wizara hiyo imesema kuwa hali hiyo imechangiwa na maandamano yanayoendelea ya kupinga mswaada wa fedha  wa mwaka 2024/2025 .

 

Wanafunzi wanaosoma shule za mjini wameanza likizo hiyo hii leo kwani sehemu nyingi mjini huenda zikashuhudia maandamano.

Wanafunzi walitarajiwa kuanza likizo fupi jumatano wiki hii kama ilivyotangazwa hapo awali hali iliyochangiwa na mvua kubwa iliyosabisha mafuriko maeneo mbalimbali nchini.

 

Written by: Susan Umazi

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online