Mtuhumiwa wa mauaji ya kikatili ya mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika eneo la Molo, Nakuru, amekamatwa baada ya msako wa polisi.
Walter Kipkoech mwenye umri wa miaka 23, alikamatwa katika kijiji cha Lagwenda, Kuresoi Kaskazini, baada ya polisi kumfuatilia kwa muda.

Kipkoech anadaiwa kumuua Joy Wangui mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Molo, ambaye mwili wake ulipatikana ndani ya nyumba eneo la Kiambaa, lokesheni ya Moto.
Polisi wanasema walipata shoka, panga na visu viwili vilivyokuwa na madoa ya damu katika eneo la tukio,kichwa cha marehemu kando pamoja na ujumbe ukutani uliyoandikwa Kwa damu ukisema ... "I love you Joy but never cheat,am sorry."
Kipkoech yuko katika Kituo cha Polisi cha Molo akisubiri kufikishwa mahakamani, huku uchunguzi ukiendelea.