TAHADHADHARI YYA WAJENZI.
By Dayo Radio
Published on 25/04/2025 13:45
News

Tahadhari imetolewa Kwa wanakandarasi wa ujenzi humu nchini kukoma kutumia bidhaa na vifaa vya ujenzi visivyo kuwa na ubora wakitaja inahatarisha usalama na maisha ya wakenya.

Akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza saruji iliyokamilika Kwa ujenzi katika kiwanda cha saruji cha bamburi, mkuu wa huduma za ubunifu na ubora wa kiufundi Fedelis sakwa amesema kwamba yeyote anayepania kuanzisha ujenzi wafwate njia sahihi zinzohitajika na wahandisi na waliobobobea Katika nyanja za ujenzi.

"Ningependa kusema wale wote wanahusika katika ujenzi wahakikishe wanatumia bidhaa bora ili kuepuka kuhatarisha maisha"

Kauli hiyo imeweza kuungwa mkono na martn kariuki ambaye ni mkurugenzi katika kitengo cha mauzo kampuni ya saruji ya bamburi na kuongeza kuwa uzinduzi wa kampuni hiyo itasaidia kubuni nafasi za ajira miongoni mwa vijana

"Ujio wa kiwanda hiki utasaidia pakubwa katika kubuni nafasi za ajira kwa vijana na huu ni mwanzo tu ila tutazidi kuwa na ushiriakiano zaidi"

Hatua hii inajiri siku chache baada ya jumba la ghorofa 11 kuporomoshwa kufwatia ujenzi uliyotumia vifaa duni.

Comments
Comment sent successfully!

Chat Online